Msanii wa Bongo Flava Yammi, hivi karibuni amekana kuwa na mahusiano na msanii kutoka Label ya WCB Wasafi Mbosso. Yammi alisema hayo akiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari pamoja na Mwijaku. Yammi na Mbosso wamedhani kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu baada ya kuonekana kwenye video mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na kuachia nyimbo ya pamoja ya “Nitadumu Nae” ambayo imefanya vizuri kwenye chart mbalimbali za muziki wa Bongo Flava.